UNITS

Mahakama ina jumla ya vitengo vinne (4)tu,vya kiutawala ambavyo ni:-

 •   KITENGO CHA FEDHA

Majukumu

 •   Kusimamia masuala ya fedha.
 •   Kusimamia masuala ya manunuzi ya taasisi .
 •    Kusimamia masuala ya malipo, mikopo na madeni ya taasisi.
 •   KITENGO CHA SERA NA MIPANGO

Majukumu

 •    Kusimamia sera, mipango na utekelezaji wa maagizo ya mipango hiyo.
 •    Kushirikiana na mwenyekiti kuandaa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi inapohitajik .
 •    Kupanga utaratibu bora wa utunzaji wa takwimu mbali mbali za mahakama.
 •    Kushirikiana na kupendekeza namna ya kupunguza kasoro za kiutendaji katika taasisi.
 •    Kupanga mipango endelevu ya shughuli za taasisi.
 •   KITENGO CHA UTUMISHI

Majukumu

 •    Usimamizi wa rasilimali watu.
 •    Usimamizi wa mali za taasisi ikiwemo majengo ya taasisi.
 •    Kusimamia mazingira bora ya kazi, majengo na wafanyakazi.
 •    Kusimamia maslahi ya wafanyakazi.
 •    Kutunza kumbukumbu sahihi za watumishi wote katika sehemu ya kazi.
 •    Kuchanganua na kukabidhi idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo ya muda mrefu na mfupi.
 •   KITENGO CHA ELIMU NA MASHAURI

Majukumu

 •    Kutoa Elimu kwa Jamii.
 •    Kuwashauri wadaawa wanapofika mahakamani.
 •    Kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi.
 •    Kusimamia na kutunza majalada na kumbukumbu za mashauri.
 •    Kuwasaidia mahakimu katika kufanya utafiti wa kisheria.
 •    Kutafuta kesi au sheria mbali mbali katika nukuu zao na katika kutayarisha maamuzi.

Chair Photo

Chairperson

Mr: Is-haka Ali Khamis

Chairperson

Katika mwezi wa Septemba 2022, Ndugu IS-HAKA ALI KHAMIS ameteuliwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi Zanzibar kuchukuwa nafasi ya ndugu Khamis R. Khamis.

  RELATED LINKS