BACKGROUND ...

Jumla ya Wenyeviti watano waliteuliwa kuiongoza Mahakama ya Ardhi katika nyakati tofauti tokea kuundwa kwake hadi muda huu.

 

MWAKA 2022 - HADI SASA

Ndugu , Is-haka Ali Khamis Katika mwezi wa Septemba 2022 ameteuliwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi Zanzibar kuchukuwa nafasi ya ndugu Khamis Rashid Khamis.

 

MWAKA 2019 - 2022

Ndugu , Khamis Rashid Khamis Katika mwezi wa Septemba 2019 ameteuliwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi Zanzibar kuchukuwa nafasi ya ndugu Faraji Shomari Juma.

 

MWAKA 2013 - 2019

Ndugu , Faraji Shomari Juma aliteuliwa kuwa mwenyekiti ambapo ndugu Saluma Hassan Bakari na ndugu Zahra Haji Hassan walikuwa manaibu wenyeviti, baadae Naibu Mwenyekiti kwa upande wa Pemba alikua ndugu Khamis Rashid Khamis aliyechukua nafasi iliyoachwa na ndugu Salum Hassan Bakari kuanzia mwezi Februari 2018 hadi Septemba 2019.

 

MWAKA 2010 - 2013

Ndugu , Haroub Shehe Pandu aliteuliwa kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Mahakama hiyo, ambapo ndugu Salum Hassan Bakari aliendlelea kua Naibu Mwenyekeiti kwa upande wa Pemba.

 

MWAKA 2006 - 2010

Ndugu , Silima Hassan Silima, (Mwalimu Silima) Huyu ni mwenyekiti wa pili wa Mahakama ya Ardhi, ambaye sambamba na mwenyekiti huyo ndugu Haroub Shehe Pandu na ndugu Salum Hassan Bakari waliteuliwa kuwa manaibu wenyeviti, Mnamo mwaka 2006.

 

MWAKA 2001 - 2006

Ndugu , Zubeir Juma Mzee ( Mwalimu Zubeir ) ni mwenyekiti wa kwanza wa Mahkama ya Ardhi Zanzibar ambae aliteuliwa kushika nafasi hiyo mnamo mwanzoni mwa mwaka 2001.

Chair Photo

Chairperson

Mr: Is-haka Ali Khamis

Chairperson

Katika mwezi wa Septemba 2022, Ndugu IS-HAKA ALI KHAMIS ameteuliwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi Zanzibar kuchukuwa nafasi ya ndugu Khamis R. Khamis.

  RELATED LINKS