BACKGROUND

Mahakama ya Ardhi Zanzibar imeanzishwa chini ya kifungu cha 3 (1) cha Sheria ya Mahakama ya Ardhi nambari 7 ya mwaka 1994 (S. 3 of the Land Tribunal Act no. 7 of 1994). Sheria hii ilitiwa saini mnamo tarehe 24/2/1995 na aliyekua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa wakati huo MHE. DK. SALMIN AMOUR JUMA.

Madhumuni makubwa ya kuanzishwa sheria hii ni kuanzisha Mahakama ya Ardhi itakayokua inasikiliza na kutolea maamuzi migogoro ya ardhi kwa haraka na ikiwezekana kwa njia ya usuluhishi. Hivyo basi Mahakama za Ardhi zimechukua mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ardhi yaliyokua yakisikilizwa na Mahakama za kawaida Unguja na Pemba, ambapo ilionekana kua, kesi hizo za ardhi zilikua zikichelewa sana kusiksilizwa na kutolewa maamuzi kiasi cha kuwepo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.

Sheria ya Mahkama ya Ardhi ya mwaka 1994, ilitambua, kuwepo kwa Hakimu mmoja tu wa kuhukumu kesi za ardhi Unguja na Pemba ambae aliitwa MWENYEKITI WA MAHAKAMA YA ARDHI. Hivyo, Mwenyekiti wa mwanzo wa Mahakama hii alikua ni Ndugu Zubeir Juma Mzee, (Mwalimu Zubeir), ambae aliteuliwa kushika nafasi hiyo mnamo mwanzoni mwa mwaka 2001. Licha ya kuwepo kwa sheria pamoja na Mwenyekiti, labda tuseme kutokana na matatizo mbali mbali yaliyokuwepo wakati huo, Mahakama hii haikuweza kufanya kazi zake hadi mwaka 2006 ikiwa chini ya Mwenyekiti wake wa pili Nd. Silima Hassan Silima, (Mwalimu Silima). Kwa upande wa Unguja, Mahakama hii ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi wa Mei 2006, na kwa upande wa Pemba, ilizinduliwa rasmi mnamo mwaka huo huo wa 2006.

Hali ya kuwepo kwa Hakimu (Mwenyekiti) mmoja tu wa kusikiliza na kutolea maamuzi mashauri ya ardhi Unguja na Pemba, pamoja na ongezeko kubwa la kesi kwenye Mahkama ya ardhi, kulisababisha kuchelewa kutatuliwa kwa mashauri ya ardhi. Kutokana na ucheleweshaji mkubwa wa utatuzi wa migogoro ya ardhi, ililazimu Serikali kuifanyia marekebisho Sheria ya Mahkama ya Ardhi mnamo mwaka 2008 kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mahakama ya Ardhi no. 1/2008 (The Land Tribunal Amendment Act No.1/2008).

Sheria hii ya marekebisho, iliruhusu kuanzishwa kwa Mahkama za Ardhi katika Mikoa yote ya Zanzibar. Aidha, iliruhusu kuwepo kwa Manaibu wenyeviti wawili wa Mahakama ambapo Naibu mmoja wa Mwenyekiti atafanya kazi Unguja na Naibu mwengine atafanya kazi Pemba. Pia Sheria hii, iliruhusu kuwepo kwa Mahakimu wa ardhi wa Mikoa kwenye Mahakama ya Ardhi mbali ya Mwenyekiti na Manaibu wenyeviti. Read More...

Chair Photo

Chairperson

Mr: Is-haka Ali Khamis

Chairperson

Katika mwezi wa Septemba 2022, Ndugu IS-HAKA ALI KHAMIS ameteuliwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi Zanzibar kuchukuwa nafasi ya ndugu Khamis R. Khamis.

  RELATED LINKS